Categories
Mwanzo

Mwanzo Utangulizi

Utangulizi

Neno “Mwanzo” linatokana na neno la Kiyunani “Geneseos” ambalo maana yake ni “Asili,” “Chimbuko,” au “Chanzo”; linatokana na tafsiri ya Agano la Kale ya Kiyunani ijulikanayo kama “Septuagint.” Kitabu hiki kinaeleza mwanzo wa ulimwengu, mwanzo wa mwanadamu (yaani mwanamke na mwanaume), mwanzo wa dhambi ya mwanadamu, mwanzo wa ahadi na mpango wa Mungu wa wokovu, na uhusiano wa kipekee kati ya Abrahamu na Mungu. Pia kinaeleza juu ya watu mahsusi wa Mungu, na mipango yake katika maisha yao. Baadhi ya watu hawa ni Adamu na Eva, Noa, Abrahamu, Isaki, Yakobo, Yosefu na ndugu zake, na wengine wengi.

Mwanzo ni kitabu cha kwanza miongoni mwa vitabu vinavyoitwa “Vitabu Vitano vya Mose” vilivyoko mwanzoni mwa Biblia. Vitabu hivi vinaitwa pia Vitabu vya Sheria kwa sababu ndipo palipoandikwa maagizo na sheria za Mungu kwa watu wa Israeli. Kitabu cha Mwanzo kama kitabu cha utangulizi kinaelezea habari za Mungu kwanza, na kuendelea kujifunua mwenyewe kwa wanadamu, ambalo ni jambo la muhimu sana. Katika kitabu hiki tunapata ahadi ya kwanza kabisa ya ukombozi wa mwanadamu aliyeanguka: “…uzao wa mwanamke utakuponda kichwa…” (

3:15

). Kitabu cha Mwanzo kinaelezea jinsi ilivyotokea hadi Israeli wakafanyika watu maalum wa Mungu.

Mwandishi

Wayahudi na Wakristo wanashikilia mwandishi ni Mose.

Kusudi

Kumfunulia mwanadamu mwanzo wa kuumbwa kwa mbingu na nchi, na vyote vilivyomo. Kumwonyesha kuwa Mungu ndiye Muumbaji pekee.

Mahali

Katika Ghuba ya Sinai, watu wa Israeli walipokuwa jangwani.

Tarehe

Kati ya 1450–1410 K.K.

Wahusika Wakuu

Adamu, Eva, Noa, Abrahamu, Sara, Isaki, Rebeka, Yakobo, Yosefu.

Wazo Kuu

Kueleza uumbaji, kuanguka kwa mwanadamu, na ahadi ya ukombozi wa mwanadamu kwa njia ya Yesu Kristo. Kila msingi mkuu wa imani katika Maandiko una mizizi yake katika Mwanzo kama asili, kitu kamili, au mfano, au ufunuo halisi.

Mambo Muhimu

Uumbaji, kuanguka kwa mwanadamu, ahadi za ukombozi wa mwanadamu kupitia Yesu Kristo.

Mgawanyo

Kuumbwa kwa ulimwengu, na mwanadamu (

1:1–2:25

)

Kuanguka kwa mwanadamu na matokeo ya dhambi (

3:1–5:32

)

Habari za Noa (

6:1–9:29

)

Kutawanywa kwa mataifa (

10:1–11:32

)

Maisha ya Abrahamu (

12:1–25:18

)

Isaki na familia yake (

25:19–26:35

)

Yakobo na wanawe (

27:1–37:1

)

Maisha ya Yosefu (

37:2–50:26

).

Categories
Mwanzo

Mwanzo 1

Siku Sita Za Uumbaji Na Sabato

1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.

2 Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.

3 Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo.

4 Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza.

5 Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

6 Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.”

7 Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo.

8 Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.

9 Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu.” Ikawa hivyo.

10 Mungu akaiita nchi kavu “ardhi,” nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.

11 Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo.

12 Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema.

13 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu.

14 Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbalimbali, siku na miaka,

15 nayo iwe mianga kwenye nafasi ya anga ya kutia nuru juu ya dunia.” Ikawa hivyo.

16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa: mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota.

17 Mungu akaiweka katika nafasi ya anga iangaze dunia,

18 itawale usiku na mchana, na ikatenganishe nuru na giza. Mungu akaona kuwa hili ni jema.

19 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya nne.

20 Mungu akasema, “Kuwepo na viumbe hai tele kwenye maji, nao ndege waruke juu ya dunia katika nafasi ya anga.”

21 Kwa hiyo Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.

22 Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni mwongezeke, mkayajaze maji ya bahari, nao ndege waongezeke katika dunia.”

23 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tano.

24 Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo.

25 Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, wanyama wa kufugwa kulingana na aina zake, na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi kulingana na aina zake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.

26 Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi.”

27 Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe,

kwa mfano wa Mungu alimuumba;

mwanaume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.”

29 Kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote, na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa chakula chenu.

30 Nao wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo.

31 Mungu akaona vyote alivyoumba, na tazama, ilikuwa vizuri sana. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya sita.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/GEN/1-e2155c5471024fd2f1588b777b15588f.mp3?version_id=1627—

Categories
Mwanzo

Mwanzo 2

1 Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo.

2 Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote.

3 Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.

Adamu Na Eva

4 Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa.

BwanaMungu alipoziumba mbingu na dunia,

5 hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwaBwanaMungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi,

6 lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi:

7 BwanaMungu alimuumba mtu kutoka mavumbiya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.

8 BasiBwanaMungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba.

9 BwanaMungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya.

10 Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne.

11 Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu.

12 (Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri, bedola na vito shohamu pia hupatikana huko.)

13 Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi.

14 Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki ya Ashuru. Mto wa nne ni Frati.

15 BwanaMungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza.

16 BwanaMungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani,

17 lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”

18 BwanaMungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”

19 BasiBwanaMungu alikuwa amefanyiza kutoka ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake.

20 Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini.

Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa.

21 HivyoBwanaMungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama.

22 KishaBwanaMungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.

23 Huyo mwanaume akasema,

“Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu

na nyama ya nyama yangu,

ataitwa ‘mwanamke,’

kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”

24 Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

25 Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/GEN/2-2d1cbbd845aaad2395f2bf2bd55363d5.mp3?version_id=1627—

Categories
Mwanzo

Mwanzo 3

Kuanguka Kwa Mwanadamu

1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambaoBwanaMungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”

2 Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini,

3 lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ”

4 Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa.

5 Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

6 Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala.

7 Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika.

8 Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti yaBwanaMungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele zaBwanaMungu katikati ya miti ya bustani.

9 LakiniBwanaMungu akamwita Adamu, “Uko wapi?”

10 Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.”

11 Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?”

12 Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala.”

13 NdipoBwanaMungu akamuuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.”

14 HivyoBwanaMungu akamwambia nyoka, “Kwa kuwa umefanya hili,

“Umelaaniwa kuliko wanyama wote

wa kufugwa na wa porini!

Utatambaa kwa tumbo lako

na kula mavumbi

siku zote za maisha yako.

15 Nami nitaweka uadui

kati yako na huyo mwanamke,

na kati ya uzao wako na wake,

yeye atakuponda kichwa,

nawe utamuuma kisigino.”

16 Kwa mwanamke akasema,

“Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako;

kwa utungu utazaa watoto.

Tamaa yako itakuwa kwa mumeo

naye atakutawala.”

17 Kwa Adamu akasema, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka kwenye mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’

“Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako,

kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo

siku zote za maisha yako.

18 Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako,

nawe utakula mimea ya shambani.

19 Kwa jasho la uso wako

utakula chakula chako

hadi utakaporudi ardhini,

kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo,

kwa kuwa wewe u mavumbi

na mavumbini wewe utarudi.”

20 Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.

21 BwanaMungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

22 KishaBwanaMungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.”

23 HivyoBwanaMungu akamfukuzia mbali kutoka Bustani ya Edeni, akalime ardhi ambamo alitolewa.

24 Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki ya Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika huku na huko kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/GEN/3-d3efac989f195a73d84da1fe1f568963.mp3?version_id=1627—

Categories
Mwanzo

Mwanzo 4

Kaini Na Abeli

1 Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada waBwananimemzaa mwanaume.”

2 Baadaye akamzaa Abeli ndugu yake.

Basi Abeli akawa mfugaji, na Kaini akawa mkulima.

3 Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwaBwana.

4 Lakini Abeli akaleta fungu nono kutoka baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake.Bwanaakamkubali Abeli pamoja na sadaka yake,

5 lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni.

6 KishaBwanaakamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni?

7 Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.”

8 Basi Kaini akamwambia ndugu yake Abeli, “Twende shambani.” Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamuua.

9 KishaBwanaakamuuliza Kaini, “Ndugu yako Abeli yuko wapi?”

Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”

10 Bwanaakasema, “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kutoka ardhini.

11 Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka ardhi, ambayo imefungua kinywa chake na kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako.

12 Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu.”

13 Kaini akamwambiaBwana, “Adhabu yangu ni zaidi ya niwezavyo kustahimili.

14 Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua.”

15 LakiniBwanaakamwambia, “La sivyo, ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi.” KishaBwanaakamwekea Kaini alama ili mtu yeyote ambaye angemwona asimuue.

16 Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele zaBwanaakaenda kuishi katika nchi ya Nodi, iliyoko mashariki ya Edeni.

17 Kaini akakutana kimwili na mkewe, naye akapata mimba na akamzaa Enoki. Wakati huo Kaini alikuwa anajenga mji, akauita Enoki jina la mtoto wake.

18 Enoki akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli, Mehuyaeli akamzaa Methushaeli, na Methushaeli akamzaa Lameki.

19 Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila.

20 Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama.

21 Kaka yake aliitwa Yubali, aliyekuwa baba wa wote wapigao zeze na filimbi.

22 Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini.

23 Lameki akawaambia wake zake,

“Ada na Sila nisikilizeni mimi;

wake wa Lameki sikieni maneno yangu.

Nimemuua mtu kwa kunijeruhi,

kijana mdogo kwa kuniumiza.

24 Kama Kaini atalipizwa kisasi mara saba,

basi Lameki itakuwa mara sabini na saba.”

25 Adamu akakutana kimwili na mke wake tena, akamzaa mwana, akamwita Sethi, akisema, “Mungu amenijalia mwana mwingine badala ya Abeli, kwa kuwa Kaini alimuua.”

26 Naye Sethi akamzaa mwana, akamwita Enoshi.

Wakati huo watu wakaanza kuliitia jina laBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/GEN/4-84fb547288756e1086109815d6509031.mp3?version_id=1627—

Categories
Mwanzo

Mwanzo 5

Kutoka Adamu Hadi Noa

1 Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu.

Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu.

2 Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.”

3 Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi.

4 Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

5 Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa.

6 Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.

7 Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

8 Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.

9 Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.

10 Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

11 Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa.

12 Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.

13 Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

14 Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.

15 Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.

16 Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

17 Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.

18 Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki.

19 Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

20 Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.

21 Enoki alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.

22 Baada ya kumzaa Methusela, Enoki alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

23 Enoki aliishi jumla ya miaka 365.

24 Enoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.

25 Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki.

26 Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

27 Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.

28 Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.

29 Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa naBwana.”

30 Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.

31 Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.

32 Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/GEN/5-1a026391c0a934a9d29f79ed31e98036.mp3?version_id=1627—

Categories
Mwanzo

Mwanzo 6

Gharika Kuu

1 Watu walipoanza kuongezeka idadi katika uso wa dunia na watoto wa kike wakazaliwa kwao,

2 wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa yeyote miongoni mwao waliyemchagua.

3 NdipoBwanaakasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.”

4 Wanefili walikuwako duniani siku hizo, na baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo.

5 Bwanaakaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu.

6 Bwanaakasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko.

7 Kwa hiyoBwanaakasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.”

8 Lakini Noa akapata kibali machoni paBwana.

9 Hivi ndivyo vizazi vya Noa.

Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu.

10 Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.

11 Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu.

12 Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao.

13 Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia.

14 Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje.

15 Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300,upana wake dhiraa hamsinina kimo chake dhiraa thelathini.

16 Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa mojajuu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu.

17 Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia.

18 Lakini Mimi nitaweka Agano langu na wewe, nawe utaingia ndani ya Safina, wewe pamoja na mke wako, wanao na wake zao.

19 Utaingiza ndani ya Safina kila aina ya kiumbe hai wawili wawili, wa kiume na wa kike, ili kuwahifadhi hai pamoja na wewe.

20 Wawili wa kila aina ya ndege, wa kila aina ya mnyama na wa kila aina ya kitambaacho ardhini watakuja kwako ili wahifadhiwe hai.

21 Utachukua kila aina ya chakula kitakacholiwa, na ukiweke akiba kama chakula kwa ajili yako na yao.”

22 Noa akafanya kila kitu kama vile Mungu alivyomwamuru.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/GEN/6-611272bc888c83c0befacf24bb734d95.mp3?version_id=1627—

Categories
Mwanzo

Mwanzo 7

1 NdipoBwanaakamwambia Noa, “Ingia katika safina wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki.

2 Uchukue wanyama saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, na wanyama wawili wawili wa kila aina walio najisi wa kiume na wa kike.

3 Pia uchukue ndege saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, ili kuhifadhi aina zao mbalimbali katika dunia yote.

4 Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini usiku na mchana, nami nitafutilia mbali kutoka uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.”

5 Noa akafanya yote kamaBwanaalivyomwamuru.

6 Noa alikuwa na miaka 600 gharika ilipokuja juu ya dunia.

7 Noa na mkewe na wanawe na wake zao wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika.

8 Jozi ya wanyama walio safi na walio najisi, ndege na viumbe vitambaavyo,

9 wa kiume na wa kike, walikuja kwa Noa wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Noa.

10 Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia.

11 Katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili mwaka wa 600 wa kuishi kwake Noa, siku hiyo ndipo chemchemi zote hata zilizo chini sana ya ardhi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa.

12 Mvua ikanyesha juu ya nchi siku arobaini usiku na mchana.

13 Siku hiyo Noa, na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao wakaingia katika ile safina.

14 Nao walikuwa pamoja na kila mnyama wa mwituni kufuatana na aina yake, wanyama wote wafugwao kufuatana na aina zao, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi kwa aina yake, na kila ndege kufuatana na aina yake, naam kila kiumbe chenye mabawa.

15 Viumbe vyote vyenye pumzi ya uhai ndani yake vikaja kwa Noa viwili viwili, vikaingia katika safina.

16 Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Noa, ndipoBwanaakamfungia ndani.

17 Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani na maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka kwenye uso wa nchi.

18 Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji.

19 Maji yakazidi kujaa juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote.

20 Maji yakaendelea kujaa yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano.

21 Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote.

22 Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa.

23 Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.

24 Maji yakaifunika dunia kwa siku 150.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/GEN/7-874c521a5d2bae9b59e933adf27e40cb.mp3?version_id=1627—

Categories
Mwanzo

Mwanzo 8

Mwisho Wa Gharika

1 Mungu akamkumbuka Noa na wanyama wote wa porini na wa kufugwa waliokuwa naye ndani ya safina, akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakaondoka.

2 Zile chemchemi zilizo chini sana ya ardhi pamoja na malango ya mafuriko ya mbinguni yakawa yamefungwa nayo mvua ikawa imekoma kunyesha kutoka angani.

3 Maji yakaendelea kupungua taratibu katika nchi. Kunako mwisho wa siku ya 150, maji yalikuwa yamepungua,

4 katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa saba, safina ikatua katika milima ya Ararati.

5 Maji yakaendelea kupungua hadi mwezi wa kumi, na siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima vikaonekana.

6 Baada ya siku arobaini Noa akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina

7 na akamtoa kunguru, akawa akiruka kwenda na kurudi mpaka maji yalipokwisha kukauka juu ya nchi.

8 Kisha akamtoa hua ili aone kama maji yameondoka juu ya uso wa ardhi.

9 Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Noa ndani ya safina. Noa akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina.

10 Noa akangojea siku saba zaidi kisha akamtoa tena hua kutoka safina.

11 Wakati hua aliporejea kwa Noa jioni, alikuwa amechukua katika mdomo wake jani bichi la mzeituni, lililochumwa wakati ule ule! Ndipo Noa akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya uso wa dunia.

12 Akangojea siku saba zaidi na akamtuma tena hua, lakini wakati huu hua hakurudi tena kwa Noa.

13 Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka 601, wa kuishi kwake Noa, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Noa akafungua mlango wa safina akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka.

14 Katika siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili dunia ilikuwa imekauka kabisa.

15 Ndipo Mungu akamwambia Noa,

16 “Toka ndani ya safina, wewe na mkeo na wanao na wake zao.

17 Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.”

18 Kwa hiyo Noa akatoka nje pamoja na mkewe, wanawe na wake zao.

19 Wanyama wote na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi na ndege wote, kila kitu kiendacho juu ya nchi, aina moja baada ya nyingine vikatoka katika safina, kila aina ya kiumbe, kimoja baada ya kingine.

Noa Atoa Dhabihu

20 Kisha Noa akamjengeaBwanamadhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama na ndege wote walio safi, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.

21 Bwanaakasikia harufu nzuri ya kupendeza, naye akasema moyoni mwake, “Kamwe sitailaani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, hata ingawa kila mwelekeo wa moyo wake ni mbaya tangu ujana. Kamwe sitaangamiza tena viumbe hai vyote kama nilivyofanya.

22 “Kwa muda dunia idumupo,

wakati wa kupanda na wa kuvuna,

wakati wa baridi na wa joto,

wakati wa kiangazi na wa masika,

usiku na mchana

kamwe havitakoma.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/GEN/8-2be6a936c3a1ee174d8e9adcb5e4b86b.mp3?version_id=1627—

Categories
Mwanzo

Mwanzo 9

Mungu Aweka Agano Na Noa

1 Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni mkaongezeke kwa idadi na mkaijaze tena dunia.

2 Wanyama wote wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi, na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu.

3 Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu.

4 “Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai.

5 Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake.

6 “Yeyote amwagaye damu ya mwanadamu,

damu yake itamwagwa na mwanadamu,

kwa kuwa katika mfano wa Mungu,

Mungu alimuumba mwanadamu.

7 Kuhusu ninyi, zaeni mwongezeke kwa wingi, mzidi katika dunia na kuijaza.”

8 Ndipo Mungu akamwambia Noa na wanawe pamoja naye:

9 “Sasa mimi ninaweka Agano langu nanyi, pamoja na uzao wenu baada yenu,

10 pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wote wa porini, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi, kila kiumbe hai duniani.

11 Ninaweka Agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika, kamwe haitakuwepo tena gharika ya kuangamiza dunia.”

12 Mungu akasema, “Hii ni ishara ya Agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, Agano kwa vizazi vyote vijavyo:

13 Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya Agano nifanyalo kati yangu na dunia.

14 Wakati wowote ninapotanda mawingu juu ya dunia na upinde wa mvua ukijitokeza mawinguni,

15 nitakumbuka Agano langu kati yangu na ninyi na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina. Kamwe maji hayatakuwa tena gharika ya kuangamiza uhai wote.

16 Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka Agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani.”

17 Hivyo Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya Agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.”

Wana Wa Noa

18 Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.)

19 Hawa ndio waliokuwa wana watatu wa Noa, kutokana nao watu walienea katika dunia.

20 Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu.

21 Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake.

22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

23 Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.

24 Noa alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea,

25 akasema,

“Alaaniwe Kanaani!

Atakuwa mtumwa wa chini sana

kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.”

26 Pia akasema,

“AbarikiweBwana, Mungu wa Shemu!

Kanaani na awe mtumwa wa Shemu.

27 Mungu na apanue mipaka ya Yafethi;

Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu,

na Kanaani na awe mtumwa wake.”

28 Baada ya gharika Noa aliishi miaka 350.

29 Noa alikuwa na jumla ya miaka 950, ndipo akafa.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/GEN/9-aeeaed3f28c8c0a6df85c2bc1ed1ad83.mp3?version_id=1627—